Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mbunge Neema Lugangira achangia pedi kwa watoto 42

Jumatano , 28th Jul , 2021

Mbunge Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (NGOs Tanzania Bara) Mhe. Neema Lugangira amewasilisha mchango wa Taulo za Kike kwa wanafunzi 42 mwaka mzima, katika Ofisi za EATV, Mikocheni ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya Namthamini.

Mbunge Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (NGOs Tanzania Bara) Mhe. Neema Lugangira (kushoto) akikabidhi mchango wake na kupokelewa na Mtangazaji wa Drive Show Justine Kessy

Akizungumza baada ya kukabidhi mchango huo amesema kuwa kampeni ya Namthamini isiishie tu kwa wanafunzi mashuleni lakini pia ifike katika Magereza ili kusaidia pia wafungwa na mahabusu wakike ambao taulo pia ni changamoto kwao.

“Nimeguswa na kampeni ya Namthamini na nimekuwa nikifanya hivyo kupitia Taasisi yangu pia kuhakikisha tunasaidia Watoto wa kike kubaki Shule hasa madarasa yale ya mitihani ili Watoto hawa wasipoteze ndoto zao”, amesema Mh. Lugangira.

Mbunge Viti Maalum CCM (NGOs Tanzania Bara) Mhe. Neema Lugangira ( wa pili kutoka kushoto )  akiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa EATV ambapo kulia ni Afisa Mahusiano wa IPP Media, Nancy Mwanyika.

Mheshimiwa Lugangira ambaye pia ni Mkurugenzi Agri Thamani amesema kuwa katika kuhakikisha pia tunathamini Viwanda vya ndani, taulo za kike pia zinatakiwa kupewa nguvu katika uzalishaji wake kwa wafanyabiashara wa ndani.

“Nimeleta taulo hizi ambazo zinatengenezwa na kiwanda cha ndani ili kusisitiza Uzalendo kwanza kwa vitendo, tuthamini vya ndani, hii imekuwa ni moja ya hoja zangu hata ninapokuwa Bungeni”, amesema Lugangira.
 

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi