Jumamosi , 3rd Feb , 2018

Mbunge wa jijini Nairobi nchini Kenya, amekamatwa kuhusiana na mzozo unaozunguka kujiapisha kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Raia Odinga kwa kile anachokitaja kama rais wa watu wa Kenya.

Mbunge wa Makadara jijini Nairobi, George Aladwa amekamatwa leo nyumbani kwake na maafisa wa idara ya upelelezi na kupelekwa hadi makao makuu ya idara hiyo kwa mahojiano zaidi.

Aladwa ambaye amewahi kuwa Meya wa jiji la Nairobi, alikuwa katika mstari wa mbele katika mipango ya sherehe hizo ambayo haikuwa na idhini ya serikali.

Mbunge mwingine wa Nairobi Tom Kajwang alikamatwa na kufikishwa mahakamani na hatimaye kuachiliwa kwa dhamana mwishoni mwa wiki hii.