Jumapili , 18th Mei , 2014

Serikali imetakiwa kupiga marufuku ngoma ya kigodoro pamoja na vazi la kangamoko ambayo imeliteka jiji la Dar es Salaam kwa madai kuwa ngoma na vazi hilo vinapotosha maadili.

Mbunge wa Lindi Mjini ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salum Barwany.

Waziri kivuli wa wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Salum Barwany, amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani kwa mwaka ujao wa fedha.

Barwany amefafanua kuwa maadili ya Kitanzania yanaendelea kuporomoka huku serikali ikishindwa kuzuia ngoma na vazi hilo alilodai kuwa ni sehemu ya vitendo vichafu vinavyochafua taswira ya nchi pamoja na kuharibu maadili ya kizazi cha sasa.