Jumatatu , 12th Feb , 2024

Mbunge wa Viti Maalum Dkt Thea Ntara, ameiomba serikali kuweka mpango wa madhubuti wa kuhakikisha elimu ya matumizi sahihi ya vidonge vya kuzuia mimba vya P2 inatolewa kwa mabinti ili kuwaepusha na madhara ya kutopata watoto baadaye.

Mbunge wa Viti Maalum Dkt Thea Ntara

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 12, 2024, Bungeni Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Afya, na swali alke lilijibiwa na Naibu Waziri Dkt Godwin Mollel.

"Hili suala sasa hivi linatisha, mabinti wanatumia hizo P2 kama wanavyotumia panado yaani hakuna utaratibu tutafika wakati mabinti hawa hawataweza kupata watoto, je serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa hao mabinti ili wajue matumizi ya P2 pamoja na hizo 'Energ drink," amehoji Mbunge Dkt Thea Ntara

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Afya amesema, "Ni kweli matumizi ovyo ya P2 yanaleta madhara mengi, inasababisha akina mama kupata hedhi ambayo haina mpangilio na wakati mwingine kupata matatizo ya mifupa, sisi wote kwa pamoja tushirikiane kuhamasisha matumizi mazuri ya P2 yanayozingatia ushauri wa kitaalamu,".