
Baada ya maswali na majibu ya leo Mbunge Mlinga aliomba mwongozo wa Spika kuhusu kitendo ambacho Mbunge wa Chadema Anatropia Theonest alikifanya cha kumvua kofia na kumkosesha haki ya kuwa ndani ya Bunge kwa kuwa kanuni za Bunge zinataka Mbunge akivaa kanzu avae na baraghashia.
Akizungumza na EATV kuhusu tuhuma hizo Mbunge Anatropia amesema ''Nilikuwa natembea haraka kwenda kwenye kikao na kofia yake iliguswa na mkono kwa kusukumana na kuokotwa na ndiyo maana alivyotoka binafsi nilimsaidia kutafuta aliyeiokota''.
Aidha Mbunge huyo amesema kwamba bado wanazidi kuwasiliana ili kujua mtu aliyeiokota na baraghashia hiyo na kuondoka nayo.
Aidha Baada ya Mbunge Mlinga kuomba mwongozo Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amesema atatoa majibu baada ya kujiridhisha na tuhuma hizo.