Alhamisi , 27th Mei , 2021

Mbunge wa Viti Maalum Nusrat Hanje, amehoji ni kwanini vijana waliomaliza darasa la saba hawapewi fursa ya kuajiriwa na taasisi za serikali hata kama wanazo fani walizozipata kupitia vyuo vya ufundi vinavyotambulika na serikali kwa kigezo cha kutokuwa na cheti cha kidato cha nne.

Mbunge wa Viti Maalum Nusrat Hanje

Kauli ameitoa Bungeni hii leo Mei 27, 2021, wakati akiuliza swali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kuiomba serikali iangalie namna ya kuwaajiri kwani hivyo vyuo vinatambulika, ambapo Waziri Mkuu alijibu kwamba tatizo la ajira ni la Dunia nzima hivyo serikali inao mkakati wa kuanzisha viwanda vitakavyoweza kutoa ajira kwa watu wote.

Tazama video hapa chini