Jumamosi , 29th Mei , 2021

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewataka wanachama wa chama hicho kuendelea kushirikiana hasa katika masuala ya kuenga chama ikiwemo ujenzi wa ofisi hali itakayowaondolea usumbufu wa kwenda kupanga nyumba binafsi.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe

Kauli hiyo ameitoa leo Mei 29, 2021, mkoani Shinyanga, mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa ofisi za chama hicho katika Jimbo hilo.

Mbowe pamoja na viongozi wengine anaendelea na ziara katika mikoa mbalimbali ikiwa ni harakati za kuendelea kukiimarisha chama hicho.