
Mkutano wa Freeman Mbowe na wanahabari
Akizungumza na wanahabari leo Mjini Dodoma Mbowe amesema hajawahi kujihusisha kwa kufanya biashara wala kutumia madawa ya kulevya wakati wote katika maisha yake.
Pia Mbowe amesema kuwa vita hiyo imechelewa sana kuanza kwani ilipaswa kuanza miaka mingi iliyopia, kwa kuwa imekuwa ikididimiza mandeleo ya Taifa.
Mbowe amesema kuwa CHADEMA inaunga mkono vita dhidi ya dawa za kulevya na iko tayari kuungana na yeyote atakayeiendesha bila kujali, lakini haiko tayari kuunga mkono vita yenye ila ndani yake.
Mbowe pia amesema atamshitaki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kumchafua kwa kuwa anaamini kuwa yeye hana hatia bila kusubiri kusafishwa na polisi.
Msikilize hapa.