
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu George Mbijima.
Mbijima amesema hayo baada ya kubaini uwepo wa wanachama wenye umri mkubwa katika kikundi cha vijana wanaojishughulisha na ufundi seremala, cha Azimio katika halmashauri ya Babati mkoani Manyara.
Mbijima ambaye alifanya uhakiki wa papo kwa papo wa umri wa vijana katika kikundi hicho ndipo alipobaini hali hiyo na kusema huenda kuna watu wengi wananufaika na fedha za serikali kinyume cha taratibu.
Baada ya kubaini hali hiyo Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge amewasihi vijana kukataa kutumika kwa vikundi vyao kwa manufaa ya watu wengine wenye lengo la kujinufaisha kupitia fedha za serikali.