Lengo la kukutana kwa viongozi hao ni kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kwa usimamizi na uratibu wa chama cha mapinduzi chini ya uenyekiti wa makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM mzee John Malechele.
Baada ya mazungumzao hayo kuanza mwezi Oktoba mwaka jana viongozi wa chama tawala cha (SPLM) ambacho kimegawanyika makundi matatu moja likiwa kundi lililoko madarakani chini ya Rais Salva Kiir.
Kundi la pili linaloongozwa na aliyekuwa makamu wa Rais Dkt Rieck Machar na la Tatu ni lile la waliokuwa wafungwa wa kisiasa wamekutana mara kadhaa jiji Arusha ambapo walikubaliana kusaini mkataba wa kumaliza mgogoro huo, zoezi ambalo hadi muda huu halijafanyika na mazungumzo yanaendelea.
Viongozi waliiwasili jijini Arusha kwa lengo la kushuhudia utiaji sahihi huo ni pamoja marais Dkt Jakaya Kikwete wa Tanzania, Uhuru Kenyata wa Kenya na Yoweri Museven wa Uganda.
Wengine ni pamoja na Makamu wa Rais Tanzania Dkt Mohamed Gharibu Bilal , Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Sirili Ramafosa, na mawaziri na watendaji wa sekta mbalimbali.