Serikali ya Tanzania imeanza kutengezeza taratibu za mazingira ya kisheria kwa wafanyabiashara wazawa na wageni, sheria ambayo itasaidia sana katika kulinda maslahi yao na yawalaji ambao ni wanunuzi wa bidhaa zao.
Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Africa Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dkt.Susan Kolimba ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa jukwaa la katibu mkuu na baraza la wafanyabiashara wa Jumuiya ya Africa Mashariki kwa kushirikiana na wasimamizi kutoka serikalini ambao wanasimamia sekta za biashara na uchumi nchini kwa lengo lakujadili namna yakutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakuta wafanyabiashara hao nakuwawekea mazingira rafiki.
Dkt Kolimba amesema serikali imeamua kuanzisha sheria hiyo ili isaidie shughuli mbalimbali zakiuchumi na kibiashara ziende kwa uwazi ambao utasaidia taifa kudhibiti mapato yake yasipotee.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa baraza la biashara nchini bwana Felix Mosha amesema ni vema serikali ianze kushughulikia mapungufu yaliyopo kwenye biashara.





