Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania Dkt Seif Rashid.
Dkt. Bukuku amesema hayo katika mkutano mkutano wa kimataifa unaowahusisha wataalamu wa fani ya baabara kutoka nchi za kati kusini na mashariki mwa afrika chini ya mwavuli wa taasisi ya APECSA unaoendelea katika makao makuu ya jumuiya ya Afrika Jijini Arusha.
Wakati huo huo Waziri wa Afya wa Tanzania Seif Idd Rashid amebainisha kuwa kwa sasa hali ya maabara katika maeneo ya mikoa nchini Tanzania imeimarika zaidi kushinda miaka iliyopita.
Wakati huo huo, serikali imesema inaendelea na utafiti kuhusu chanjo ya ukimwi huku lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha kuwa inatokomeza maambukizi mapya pamoja na upatikanaji wa tiba ya kudumu kwa waathirika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Donald Mbando amefafanua kuwa kwa sasa utafiti kuhusu chanjo hiyo unafanyika katika mikoa ya Mbeya, Kagera, Dar es Salaam na Kilimanjaro na kuwa imefikia katika awamu ya tatu ambayo inahusisha binadamu ingawaje bado idadi kamili ya waliofanyiwa utafiti na matokeo yake haijatolewa.
Aidha, Dkt Mbando ametoa wito kwa wadau wa maendeleo kutekeleza dhima ya taasisi zao ili kuchangia maendeleo hasa katika tafiti zinazohusu upatikanaji wa tiba za magonjwa yasio na tiba nchini Tanzania.