Ijumaa , 8th Jul , 2016

Matumizi ya samaki duniani yameongezeka zaidi ya kilo 20 kwa mwaka kwa mara ya kwanza, imesema ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani, FAO.

Picha hii ya maktaba inawaonyesha wavuvi wakirejea pwani baada ya shughuli ya kuvua samaki.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyochapishwa leo ongezeko hilo la matumizi ya kila mtu yanatokana na usambazaji imara wa samaki na mahitaji ya baadhi ya aina za samaki, sanjari na uhifadhi wa samaki hao.

Hata hivyo FAO inasema licha ya hatua hizo kubwa lakini bado raslimali za majini hazijaimarika, na takribani theluthi moja ya akiba ya samaki wa biashara sasa wanavuliwa katika kiwango kisicho endelevu ikiwa ni mara tatu zaidi ya ilivyokuwa mwaka 1974.

Manuel Barange ni Mkurugenzi wa FAO kitengo cha sera na rasilimali za uvuvi, anafafanua juu ya ongezeko hilo la matumizi ya samaki limetokana na watu milioni 57 ambao walishiriki uvuvi kama kazi ya msingi,

Aidha, Mkurugenzi huyo amesema kuwa uuzaji wa samaki umepanda hadi kufikia dola bilioni 148 huku mauzo ya dola bilioni 80 ni kutoka nchi zinazoendelea kwa hiyo samaki sio tu chakula kwa jamii hizo bali pia inaongeza pato la taifa kwa mauzo ya nje.