![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2016/08/18/efd-machine.jpg?itok=QWcfN61k×tamp=1473970187)
Mashine za EFD
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi kutoka TRA bwana Richard Kayombo amesema kumekuwa na malalamiko kutoka wafanyabiashara kuwa wamekuwa wakitozwa pesa ya matengenezo na wasambazaji wa mashine hizo jambo linalowakatisha tamaa kuendelea kutumia machine hizo.
Hata hivyo Kayombo amesema kuwa kama matengenezo yatahusiana na uharibifu uliotokana na uzembe wa mtumiaji, atalazimika kulipia gharama za matengenezo.
"Kama imeharibika kwa uzembe wako mfano umeiangusha nchini, au imetumbukia kwenye maji, ni lazima ulipie, kwahiyo ni jukumu lako kuwa lakini, lakini kama ni matatizo yanayohufu mfumo wenyewe au msambazi, basi hakuna mtu atakayelipishwa" Amesema Kayombo
Kuhusu malalamiko ya mashine kutokuwa na mtandao (network), Kayombo amesema licha ya kwamba mashine hizo huwa zimeuganishwa katika mtandao maalum, zoezi la kutoa risiti halihitaji mtandao, hivyo amesema pasiwe na kisingizio kama hicho kama njia ya kukwepa kutoa risiti.
Kayombo pia amepongeza jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli za kuhamasisha watanzania kulipa kodi kwa hiari, kuwa sasa mwamko wa watu umekuwa mkubwa, na mwitikio ni mzuri kwa kuwa watu wanaona matumizi ya kodi yao.
Ameendelea kutoa onyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiotumia mashine za EFD, lakini pia wateja wasiokuwa na tabia ya kudai risiti, akiwataka kubadilika mapema kwa hiari yao kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.
"Kuna watu bado hawapendi kudai risiti, hata wakipewa hawataki, mfano kwenye vituo vya mafuta vilivyo vingi, kuna mashine za EFD, mtu akinunua mafuta akipewa risiti anaikataa au kuiacha hapohapo kituoni, jambo ambalo limelalamikiwa na wauzaji kwa kusababisha uchafu," Amesema Kayombo.
Amesema watu wa aina hiyo wakikamatwa, wakikamatwa, hatua ya kwanza ni kupewa onyo, hatua ya pili ni kufikishwa mahakamani na hatua ya tatu ni kufungiwa biashara kwa upande wa wafanya bishara.
![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/2016/08/18/kayombo.jpg?itok=wQxTIetb)