Alhamisi , 15th Aug , 2019

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema jeshi la polisi mkoani humo linawashikilia watu takribani tisa wanaojihusisha na utapeli kwa njia ya simu kupitia jumbe mbalimbali za maandishi.

Kamanda Nyigesa amesema watu hao walikamatwa siku ya Agosti 13, katika Tarafa ya Yombo wilayani Bagamoyo mkoani humo wakiwa na orodha ya majina na namba za watu.

Inadaiwa majina na namba hizo walizokamatwa nazo zilikuwa ni kwa ajili ya kuwatapeli watu wapya na ambao wamekwishatapeliwa.

Pia watu hao walikutwa na  simu 13 ndogo za tochi, Simu janja nne pamoja na laini 22 za
simu za makampuni mbalimbali.