Jumamosi , 19th Jul , 2014

Watu zaidi ya milioni 13 ambao wanaokabiliwa na umasikini mkubwa nchini watanufaika katika mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na serikali ya Tanzania, benki ya dunia na wadau wengine wa maendeleo.

Baadhi ya kaya Masikini mkoani Mara nchini Tanzania

Watu zaidi ya milioni 13 ambao wanakabiliwa na umasikini mkubwa nchini watanufaika katika mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na serikali ya Tanzania, benki ya dunia na wadau wengine wa maendeleo.
 
Mpango huo wa miaka kumi ambao unasimamiwa na ofisi ya Rais kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF awamu ya tatu umeanza kutekelezwa katika baadhi ya mikoa nchini.
 
Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa TASAF ambaye pia ni mkurugenzi wa fedha wa mfuko huo Bw Issaya Wambura, akizungumza baada ya kuzinduliwa kwa mpango huo wilayani Tarime,  amesema kuwa kiasi cha zaidi ya dola milioni tatu kitatumika kila mwaka ambapo walengwa watapatiwa ruzuku maalum kwaajili ya kujikimu kimaisha, elimu, afya na huduma nyingine za jamii.

Hata hivyo Bw Wambura amesema kuwa vigezo vya kitaifa vitatumika kuwabainisha walengwa katika mpango huo kisha kupitishwa na mikutano mikuu ya vijiji kwa kuzingatia vigezo hizo huku akisema kaya ambazo zimekumbwa na mapigano ya koo wilayani Tarime nazo zinaweza kunufaika endapo zitakidhi vigezo hivyo.