Jumatano , 8th Jul , 2015

Mashirika binafsi yametakaiwa kuinga mkono serikali katika kukamilisha ujenzi wa maaraba nchini ili kufanikisha zoezi hilo kwa ajili ya kuboresha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni PPF kanda ya Ziwa Meshaki Bandawe.

Akiongea Wilayani Misenyi mkoani Kagera wakati akikabidhi mifuko ya sementi katika shule ya sekondari Nkenge na Nsunga Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni PPF kanda ya Ziwa Meshaki Bandawe amesema kutoka na hali mbaya ya kiuchumi uchangiaji wa wananchi umekua unasuasua

Meshaki amesema ili kutengeneza vijana ambao wataweza kuingia katika soko la ajira la kimataifa ni lazima sekta binafsi ziweke juhudu katika kusaidia sekta ya elimu ili kutoa wataalamu mbalimbali hasa katika tasnia ya Sayansi.

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Nsunga Willium Ashimba amesema pamoja na kutokuwepo kwa maabara na walimu katika shule hiyo lakini wamefanikiwa kufaulisha Wanafunzi kwa masomo ya sayansi na endapo maabara hiyo ikikamilika itasaidia kuokoa wimbi la wanafunzi wanaofeli masomo hayo.