Alhamisi , 5th Oct , 2023

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini (NGO’s) kuhakikisha hayatumiki kuharibu maadili ya Tanzania kwa kutekeleza ajenda binafsi zisizofaa na kuzitaka kuwajibika katika kutunza na kulinda maadili kwa kuheshimu mila, desturi na tamaduni

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango

za kitanzania wakati wa utekelezaji wa programu mbalimbali.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifunga jukwaa la tatu la mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) llililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.

Aidha amewataka kuzingatia sheria za nchi na kufuata miongozo mbalimbali inayoratibu shughuli za mashirika hayo.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii kufanya uchambuzi makini wa mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuishauri serikali ipasavyo juu mwenendo na ufanisi wa mashirika hayo.

Pia Makamu wa Rais amesema suala la mabadiliko ya tabianchi linapaswa kuchukuliwa kwa umuhimu mkubwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwani Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa isiyotabirika.

Amesema serikali Serikali ingependa kuona ushiriki zaidi wa NGOs katika utoaji elimu na hamasa kuhusu uhifadhi wa mazingira, udhibiti wa majanga na maisha endelevu, utunzaji wa misitu na uoto wa asili na kuchangia katika utengenezaji au uboreshaji wa sera mbalimbali.