Jumanne , 29th Nov , 2016

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amepiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Novemba 29,

Rais Magufuli ametangaza marufuku hiyo leo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika gereza la Ukonga jiini Dar es Salaam

Ametangaza hatua hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kwamba wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi nchini na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi ya hapa nchini.

Mkuu wa gereza la Ukonga akieleza changamoto za kazi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli  alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016

 

Kadhalika Rais Magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika.

Aidha Rais Magufuli ametoa shilingi Bilioni Kumi kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Ukonga.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akichukua maelezo kutoka kwa  maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016

 

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisaini kitabu cha wageni akiwa na  Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016