Jumatano , 6th Jul , 2016

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema usalama katika kipindi hichi cha Sikukuu kwa mkoa huo umehimarika.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema usalama katika kipindi hichi cha sikukuu kwa mkoa huo umehimarika kwa maeneo mbalimbali na tayari askari wa usalama wameanza kufanya kazi.

Kamanda Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na East Africa Radio wakati akifafanua kuhusu hali ya usalama ilivyo kwa sasa hasa maeneo mbalimbali ya mikusanyiko ya watu kama Misikiti,kumbi za starehe na fukwe za Bahari sambamba na hilo amepiga marufuku kufanyika kwa Disco Toto.

Amesema jeshi la Polisi kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wamekubaliana kwa pamoja kuhakikisha wanasimamia usalama wa Jiji kuanzia ngazi ya mitaa hadi mkoa hasa nyakati za usiku.

Kamanda Sirro amewataka wananchi kutii sheria bila shuruti kwakuwa usalama wa nchi niwa kila mtanzania anawajibu wakusimamia.