
Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry imesema serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania ikiwa ni pamoja na kuimarisha demokrasia, kuimarisha usalama katika eneo la ukanda na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Taarifa hiyo imeainisha kuwa kwa niaba ya Rais wa Marekani Barak Obama na wananchi wa Marekani wanawapongeza wanainchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walivyoendesha uchaguzi wa Rais na wabunge na kudumisha rekodi ya kidemokrasia.
Hata hivyo taarifa ya waziri Kerry imeshangazwa na tamko la tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi na kuutaka uongozi mpya ulioingia madarakani kuhakikisha matakwa ya watu wa Zanzibar yanaheshimiwa.