Jumatatu , 9th Oct , 2023

Watu wasiopungua 23 wameuawa katika maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa katika mji mkuu wa Cameroon Yaoundé, huduma za dharura zimesema.

Kituo kimoja cha redio nchini humo kimesema idadi ya watu waliofariki ni 40, ikisema kuwa watu wengi bado hawajulikani waliko.

Juhudi za uokoaji zilitatizwa na mafuriko, na kuwalazimisha wenyeji kutoa miili kutoka kwenye vifusi kwa mikono yao wazi.

Mvua kubwa ilisababisha mto Mefou kupasuka kingo zake siku ya Jumapili, na kufurika katika vitongoji kadhaa.

Janga hilo linatokea karibu mwaka mmoja baada ya watu wasiopungua 14 kupoteza maisha katika maporomoko mengine ya ardhi katika mji huo.

Eneo maskini la Mbankolo liliathirika zaidi katika janga la hivi karibuni, huku baadhi ya nyumba, zikijengwa kwenye mteremko, kuporomoka na migomba  kusombwa.

Miili ya watoto "ilitapakaa katika ardhi iliyolowa", mkazi mmoja alinukuliwa akisema na tovuti ya habari ya Cameroon Voice.