Ijumaa , 30th Sep , 2022

Kunasikika milio mikubwa ya risasi nchini Burkina Faso  katika mji mkuu  Ouagadougou huku kukiwa na taarifa kwamba Televisheni ya Taifa imezimwa. Baadhi ya barabara zimefungwa kwenye mji huo mkuu huku mitandao ya kijamii ikisema kwamba huenda kuna mapinduzi yanafanyika.

Kw mujibu wa BBC inaonekana jaribio la mapinduzi linachukua hatamu kwa sasa. Milio ya risasi inasikika karibu na makazi ya Rais huku maeneo nyeti kama  bunge, Televisheni ya Taifa na makazi ya Waziri mkuu yakizuiwa na magari ya kijeshi. 

Inakumbukwa ni mwezi Januari mwaka huu ambapo kiongozi wa Taifa hilo kwa sasa  Lt Col Paul-Henri Damiba, alipompindua Rais Roch Kaboré  na kutwaa madaraka ya kijeshi.

 Jana mamia ya waandamanaji waliingia mitaani huko magharibi mwa jiji la  Bobo Dioulasso wakitaka kiongozi huyo wa kijeshi ajiuzulu wakimlaumu kwa ukosefu wa usalama nchini humo.  

Mashuhuda wanasema kwamba wanaona vikosi vya kijeshi vikizunguka nchini humo , ambapo shule zimefungwa na wananchi wakisalia dnani kusubiria taaarifa za habari .