Inadaiwa mnamo tarehe 28 mwezi huu mapacha hao walienda kuogelea kwenye fukwe za mwalo wa Mihama wilayani Ilemela jijini Mwanza ndipo wakakwama kwenye mapango ya miamba yaliyopo ndani ya ziwa Victoria na kupelekea kupoteza Maisha
“Ndani ya Maji kulikuwa na mapango ya miamba hivyo waliogolea hadi wakachoka na kushindwa kutoka na wote wakaishiwa nguvu na wote wakazama ndani ya mapango hayo na kupuiteza Maisha na sisi tulipofika tuliwatafuta na kuwakuta wamekwama kwenye mapango hayo ndipo
tukawatoa” Amesema msaidizi wa kitengo cha uzamiaji jeshi la zimamoto na uokoaji Mwanza Samweli Nyandito
Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Mwanza kamila Labani amewataka wakazi wa maeneo hayo kuacha kuogelea katika eneo hilo kutokana kuwa na hatari kufuatia uwepo wa mapango ya miamba ndani ya mwalo huo ambayo ni hatari kwao
“Natoa rai kwa wananchi wote wa mkoa wa Mwanza wanaopenda kutumia fukwe kuogelea na siyo fukwe tu hata mabwawa maalum ambayo yanatumika kuogelea wasiende kuogelea bila kufuata kanuni za usalama amabzo ni pamoja na kuvaa makoti maalum yanayomsaidia mtu kuweza kuelea yanitwa lifejacket lakini kamwe wasiogelee kama hakuna mtaalamu wa kuwasaidia kama likitokea tatizo lolote’