Alhamisi , 14th Jan , 2016

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imetupilia mbali maombi ya zuio la muda la uchaguzi wa mameya katika manispaa ya Kinondoni na Ilala jijini Dar es slaam.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na mkazi wa jijini Dar es salaam Bw. Elias Nawela kwa hati ya dharura bila kuonesha uharaka wa kusikilizwa kwa kesi hiyo na kufanya uchaguzi huo kushindwa kufanyika.

Hakimu mkazi mkuu Respicius Mijage amesema kuwa kesi za uchaguzi zinakuwa na maslahi makubwa kwa umma hivyo hata mlalamikaji hakuonesha muda wa usikilizwaji wake.

Baada ya uamuzi huo wa hakimu Mwijage, mlalamikaji Bw. Nawela amekubali maamuzi ya hakimu kwa kuwa uchaguzi huo una maslahi makubwa kwa watu wengi.

Kwa uamuzi huo sasa mahakama imezitaka manispaa hizo kuendelea na mchakato wa uchaguzi kama ilivyopangwa.

Ikumbukwe kuwa baada ya kutokea kwa sintofahamu kwa uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. George Simbachawene alimuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha uchaguzi huo unakamilika kabla ya Januari 16 2016.