Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba, 2, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kumekucha cha ITV, na kuongeza kuwa kitendo cha wao kuendelea kukaa jijini Dar es salaam, ni makosa kwa sababu hawajashindwa jijini humo.
"Walioshindwa warudi majimboni mwao kwa sababu hawajashindwa hapa, tungependa tubaki na waliokuwa wanagombea nafasi zao na wafuate taratibu, oparesheni bado inaendelea na wote hawa ambao wametoka mikoani na wako Dar es Salaam hapa ikiwemo akina Sugu tunaendelea kuwafuatilia na ndani ya muda mfupi tutawatia mbaroni", amesema SACP Mambosasa.
Aidha Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa, "Uharamu wa maandamano haya hawakutoa taarifa kwa jeshi la polisi, badala yake wanahamasishana chini kwa chini kufanya maandamano na kufunga barabara za jiji ili wananchi washindwe kufanya shughuli zao, hakuna atakayeruhusiwa kufanya mikusanyiko wala maandamano yasiyo halali".