Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mama Kanumba atumiwa ujumbe kuhusu Lulu

Ijumaa , 17th Nov , 2017

Mwanamuziki na Muigizaji nchini, Patcho Mwamba ameifungukia kauli ya Mama Kanumba ya kushukuru kitendo cha Muigizaji Lulu kufungwa miaka miwili kwa kosa la kumuua bila kukusudia muigizaji Kanumba na kusema kwamba hakuna haja ya kuendelea na 'beef' 

kwani hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba hai.

Patcho ambaye alikuwa muigizaji na rafiki wa karibu na Marehemu Steven Kanumba amesema kwamba Mama kanumba anapaswa  kuwa na moyo wa kusamehe kwa sababu binti huyo akimaliza kifungo atarudi mtaani na ataendelea na maisha yake hivyo kujengeana chuki siyo jambo jema.

"Sina la kusema juu ya jukumu ya Lulu, lakini Mahakama imeamua kama ilivyoamua, kwa upande mmoja kuna unafuu kwani kwa kesi ile kufungwa miaka miwili ni bahati, ukija upande wa pili inaumiza sana kwani jela siyo sehemu nzuri sana kwa mtu kuwepo kila mtu anajua hilo hasa ukizingatia   bado ni mdogo hivyo tumuombee Mungu ampe nguvu, uwezo naamsaidie aweze kustahimili hiyo hali" Patcho.

Aidha Patcho ameongeza "Nimemuona mama anasema anashukuru (Mama Kanumba) haki imetendeka, mimi sidhani kama kunahitajika kuwepo na ma Beef. Mwanaye, ambaye pia ni rafiki yetu ameondoka lakini tunaamini ni mipango ya Mungu. Hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba aishi. kusema naenda kumzika Kanumba upya sidhani kama kuna haja ya kuendeleza ma beef japo yapo. End of the day Lulu atatoka wataongea vizuri?. Sidhani yule mama yangu hivyo simshauri aendee kuwa na kinyongo".

Patcho amemalizia na kusema kwamba "Kusema kufungwa kwa Lulu kutampatia unafuu sidhani  ni uongo yeye aendelee kuwa mama maana ninachoamini Lulu hakumuua Kanumba bali alikuwa shahidi wakati Kanumba anakufa  ndichi ninachokiamini. Baadaye Lulu atatoka jela je  ukimuon utamgonga na gari? au Mama Lulu utaweza kuongea naye na wale ni Wahaya ni kabila moja. Sidhani kama Lulu alikuwa akikaa na kufikiria ipo siku atamuua Kanumba".

HABARI ZAIDI

Rajab Abrahaman Abdalah, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga

CCM Tanga yaijibu CHADEMA kuhusu huduma za kijamii

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama

Wazazi simamieni maadili kwa watoto 

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu