Alhamisi , 10th Nov , 2016

Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA katika kipindi cha mwezi oktoba 2016 imekusanya zaidi ya shilingi trilioni 1.15  na kufanya makusanyo yote kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kufikia zaidi ya shilingi trilioni 4 toka mwaka wa fedha kuanza  hadi sasa.

Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amesema kuwa  pamoja na mafanikio hayo ya kodi TRA vilevile imepata mafanikio katika rufaa za kesi zinazowasilishwa kwa uamuzi kwenye baraza la rufani  za kodi na kushinda kesi tisa zenye thamani ya shilingi bilioni 16.94.

 Katika hatua nyingine Mamlaka ya Mapato Tanzania imeanzisha vituo vinavyohama ili kukabiliana na msongamano wa wananchi wanao hakiki na kuboresha Taarifa za namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi-TIN kwenye mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha, Kayombo amewasisitiza wananchi wanaohakiki taarifa zao kuwa makini kwani TRA imebaini  kuibuka wananchi wasiowaaminifu ambao wanatumia mwanya wa msongamano wa wananchi kwenye vituo vya uhakiki kuwalaghai na kusababisha usumbufu uio wa lazima