Picha ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni moja ya kumbukumbu muhimu zinazopaswa kutunzwa.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa nchini Profesa Audax Mabulla amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu kumbukumbu za mambo ya kale ikiwemo misafara wa iliyokuwa vita ya kwanza ya dunia iliyopiganwa kati ya mwaka 1914 hadi 1918.
Profesa Mabulla amesema kizazi cha sasa hususani wanafunzi hawafahamu mambo mengi juu ya historia na utamaduni wa nchi yao na kwamba kuna haja ya kuweka taarifa hizo ndani ya mitaala ili waweze kuona umuhimu wake katika kutunza kumbukumbu hizo zisipotee kwa faida ya vizazi vijavyo.
Profesa Mabulla amesema Tanzania ina taarifa na kumbukumbu nyingi za kale ambazo zinahitaji kutunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kumbukumbu kwa vizazi vijavyo na kwamba ni kwa kupitia uwepo wa mitaala wanafunzi watafahamu umuhimu huu na kuupa kipaumbele.
Ametolea mfano wa nchi za Ulaya ambako kila mgeni anayeingia huko hutakiwa kwenda kutembelea Makumbusho ya nchi hizo kwani huko ndiko mahali kwenye taarifa zitakazoweza kuwafanya wageni wafahamu histori, utamaduni na kila aina ya taarifa wanayotaka kuifahamu.