Mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase,
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase, wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili utekelezaji wa mradi wa LTIP katika Halmashauri ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya
"Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mradi huu utakaopelekea vijiji vyote katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kuwa na mpango wa matumizi ya ardhi ambapo hapo awali vijiji 3 kati ya 93 vilikuwa na mpango huo lakini kwa kupitia mradi huu vijiji vyote 90 vilivyobakia vitanufaika kuandaliwa mpango wa matumizi ya ardhi," amesema DC Manase
Aidha, amesema uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kwa upande wa vijijini pamoja na urasimishaji makazi kwa upande wa mjini utapelekea kupunguza au kumaliza kabisa migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.