Jumatatu , 3rd Aug , 2020

Makatibu Wakuu na Manaibu Wanasheria wa Nchi za Jumuiya ya SADC pamoja na maafisa waandamizi wa vitengo vya sheria wameazimia kupunguza mlolongo wa taratibu zinazopelekea kuchelewesha kuridhia baadhi mambo wanayokubaliana kwenye vikao.

Akitatoa taarifa fupi ya yaliyojadiliwa kwenye Kikao chao hicho Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema nchi wanachama wamekuwa na kasi ndogo katika kuridhia baadhi ya mambo kutokana na mifumo ya nchi husika.

Amesema kutokana na nchi wanachama kuhitaji amani na usalama suala la uingizwaji na usambazaji wa silaha kwa njia za haramu limeonekana kutokukubalika kwa kila nchi wanachama.

Kuhitimishwa kwa kikao hicho kinatoa fursa ya kuanza kwa kikao kingine cha mawaziri wa nchi wanachama wa SADC ili kuchochea kasi ya maridhiano kwa ngazi za juu zaidi za maamuzi.