Ijumaa , 10th Jun , 2016

Tafiti za magonjwa yasiyo ya kuambukiza, mifumo ya afya, huduma za madawa pamoja na dawa za jadi na dawa mbadala zinatarajiwa kuwasilishwa na chuo kikuu cha afya ya sayansi Muhimbili kwa lengo la kuboresha sekta ya afya nchini.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, kuhusiana na kongamano la nne la kisayansi, Mkuu wa chuo cha MUHAS Prof. Ephata Kaaya amesema tafiti hizo zilifanywa ndani na nje ya nchi kwa kuhusisha wataalum mbalimbali katika sekta nzima ya afya

Prof. Kaaya amesema, nchi za Japan, Nigeria, Ethiopia, Uganda, Sweden, Kenya,Norway, China na Marekani watahudhuria uwasilishwaji wa tafiti hizo na kuangalia mwendeno wa tiba, kinga na uchunguzi wa saratani pamoja na matatizo yatokanayo na dawa za kulevya.

Makamu wa rais mama Samia Suluu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni kuwekeza katika afya na elimu ili kuleta maendeleo endelevu