Jumanne , 11th Jun , 2024

Watu wote tisa waliokuwemo katika ndege iliyombeba Makamu wa Rais wa Malawi Dkt.Saulos Chilima wamefariki dunia baada ndege hiyo kuanguka katika msitu wa Chikangawa.

Makamu wa Rais wa Malawi Dkt.Saulos Chilima aliyefariki dunia

Kufuatia ajali hiyo, Rais Lazarus Chakwera ametoa pole kwa familia na ndugu waliopoteza wapendwa wao na bendera za nchi hiyo zitapepea nusu mlingoti hadi mazishi yatakapofanyika.

Dkt.Chilima amekuwa Makamu wa Rais wa Malawi tangu mwaka 2020.