
Dk. Bilal amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akipanda miti ikiwa ni sehemu ya kampeni ya upandaji miti kitaifa inayofanywa kila tarehe moja ya mwezi wa nne ikiwa na lengo la kuhamasisha upandaji miti angalau katika vipindi vyote vya mvua ili kulinusuru taifa kukumbwa na majanga.
Akizungumzia mabadiliko yatabia nchi kwa dunia nzima Dk. Bilal amesema kila nchi ina njia zake za kujipanga kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea na ndio sababu kubwa unakuta nchi nyingine zinakumbwa na mafuriko, Ukame na nyingine zinakumbwa na joto kali na kusema Watanzania wakishindwa kuelewa hilo nchi itajikuta pabaya.