Jumatano , 30th Sep , 2015

Meneja wa Huduma za Utalii nchini Philip Chitaonga ameyataka Makampuni ya Utalii nchini kuchangamkia fursa ya kushiriki kwenye maonesho ya Swahili ili kujifunza njia mpya za kufanyabiashara ya utalii.

Wenyeviti na Wajumbe wateule wa vyombo vitatu, Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania, Mamlaka ya Rufaa na Kamati ya Ushauri wa Kitaalam.

Akiongea ofisini kwake Meneja huyo amesema kuwa katika maonesho hayo Mwenyekiti wa Umoja wa Mawakala wa Utalii Marekani, Terry Deo akishirikiana na mtoa mada kutoka nchini China watatoa mafunzo ya utalii na namna bora ya kufanya biashara ya utalii hivyo basi wafanyabiashara watanufaika na kubadilishana uzoefu na wafanyabiashara wenzao kutoka mataifa ya Marekani na China.

Chitaonga ameongeza kuwa uwepo wa wasilishaji mada hao utaleta chachu ya ufanyaji wa biashara ya utalii nchini Tanzania kutokana na ujuzi wa wawasilishaji mada hao walionao kutoka mataifa waliyotoka.

Maonesho ya Swahili Inter Tourism Expro yanatarajiwa kufanyika tarehe moja mpaka tarehe tatu mwezi wa kumi ambapo wageni kutoka nchi mbalimbali wameanza kuwasili ili kuangalia vivutio vya utalii vilivyomo nchini Tanzania.