Jumanne , 30th Jun , 2015

Tatizo la ajira na umaskini miongoni mwa watanzania ni baadhi ya mambo yanayotarajwa kutatuliwa iwapo January Makamba atapewa ridhaa ya kugombea nafasi ya uraisi kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.

Naibu Waziri wa Sayansi Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ambae pia Mtangaza nia ya kugombea nafasi ndani ya chama cha Mapinduzi.

Aidha ameahidi kuwa atahakikisha kwamba madini ya Tanzanite ambayo yanatoroshwa kutoka hapa nchini yataimarishwa kwa kujenga kiwanda cha kuyaboresha na soko maalum jijini humo ili kuhakikisha wameongeza thamani ya madini hayo lakini pia kutengeneza ajira kwa watanzania.

Hayo amesema jijini Arusha alipo kukutana na wana CCM kwa mkoa wa Arusha na kuomba udhamini wao katika ugombezi huo ambapo takribani wadhamini elfu mbili na ishirini na tano walijitokeza na kusaini fomu ya udmanini.

Akihutubia wananchi waliojitokeza katika ukumbi wa CCM mkoa jijini Arusha, Makamba amehimiza umuhimu wa watia nia wengine kuheshimiana mmoja na mwingine na kujenga tabia ya kuhubiri amani na umoja kwa sababu kugombea sio kugombana na kuchafuana sio dawa kwani kufanya hivo ni kuchafua chama na kujishusha hadhi na nafasi hiyo haiwakufai kwa sababu hiyo ni nafasi ya heshima na inatakiwa kuombwa kwa adabu.