Ijumaa , 7th Jun , 2024

Wananchi wa Kijiji na Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni Mkoani Singida wamefurahishwa baada ya kuona maji yakitoka bombani.

Wakazi wa Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni Mkoani Singida

Wamesema kuwa Vijiji vingi katika Tarafa hiyo iliyopo ukanda wa bonde la ufa hawajawahi kuona maji wengine tangu wazaliwe mpaka wanazeeka hatimaye kwa mara kwanza ndio wanaona maji safi na salama yakitoka bombani ambapo hapo awali walikuwa wakitumia maji ya visima.

"Yaani tulianza watoto wadogo tunambiwa maji, maji sijui wamepita wabunge wangapi tunaambiwa maji maji mpaka sasa hivi nimezeeka ndio kuja kupata maji haya, tulikuwa tunachota visima kule kinaitwa kwa Mikaeli mbali huko tunajitwisha na mtoto mgongoni na kidumu kingine cha lita tano mkononi."alisema Rozina Laurent mkazi wa Kijiji cha Lisilile

Maji hayo ni ya mradi Kintinku-Lusilile wa Vijiji 11  uliyochukua miaka kadhaa uliyogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 13 ambapo unatarajiwa kukamilika tarehe 31 mwezi huu wa June Kwa baadhi ya kazi zilizobaki.