Ijumaa , 5th Aug , 2016

Mofisa wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa kitengo cha haki za binaadamu wamelishutumu jeshi la Sudan Kusini kwa mauaji ya kikabila na ubakaji yanayoendelea katika kipindi cha mapigano ya hivi karibuni katika mji mkuu wa Juba.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir

Zeid Ra'ad Al Hussein askari mwaminifu kwa Rais Salva Kiir, kutoka kabila la Dinka, wao wamekuwa wakiwakusudia hasa watu wa kabila la Nuer huku Mpinzani mkuu wa Rais Salva Kiir, Riek Machar yeye anatoka katika kabila lengwa la Neur.

Zeid Ra'ad Al Hussein, amesema mvutano bado ni mkubwa na ukiukaji unaendelea Juba na katika maeneo mengine ya nchi hiyo.

Mkuu huyo wa haki za binadamu amewasilisha ripoti kwa baraza la usalama ya matokeo ya awali ya uchunguzi wa siku tano za mapigano yaliyoanza mji mkuu Juba Julai 7 na matokeo ya machafuko hayo.