Alhamisi , 23rd Jun , 2022

Majeruhi 6 kati ya 132 wa ajali ya Treni iliyotokea jana Juni 22, 2022, katika eneo la Malolo mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu wanne wamesafirishwa kwa rufaa kutoka Hospitali ya mkoa wa Tabora  Kitete  kwenda Bugando kwa ajili ya  matibabu zaidi.

Mabehewa ya abiria yaliyoanguka

Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani, amesema hali ya majeruhi waliowengi  maendeleo yao ni mazuri na wengine wameruhusiwa kabisa kutoka katika hospitali ,huku akitaja majeruhi 6 wenyewe wamesafirishwa kwenda mkoani Mwanza.

Hata hivyo zoezi la kuwasafirisha abiria zaidi ya 900 walionusurika katika ajali ya Treni hiyo hapo jana ambayo ilikuwa ikitoka mkoa wa Kigoma kupitia Tabora mpaka Dar es Salaam, limefanyika usiku wa jana huku chanzo cha ajali kikielezwa kuwa ni  kukatika kwa kipande kimoja cha reli na hivyo kusababisha mabehewa  8  ya abiria kuanguka .