Jumanne , 15th Apr , 2014

Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia benki ya Barclays tawi la Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kupora kiasi kikubwa cha fedha ambazo idadi yake haijajulikana mara moja.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa nne kamili katika tawi la benki hiyo iliyopo Kinondoni eneo la Bakwata likihusisha watu watatu waliokuwa na pikipiki mmoja wao akiwa na bastola.

Katika tukio hilo, mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni mfanyakazi wa benki hiyo alionekana akikimbizwa hospitali kutokana na kupata majeraha sehemu za mkononi ambapo hadi East Africa Radio inaondoka eneo la tukio, tayari kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Camilius Wambura alikuwa ameshawasili eneo la tukio na kuahidi kulitolea taarifa rasmi baada ya uchunguzi kukamilika.