Jumanne , 16th Nov , 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atapeleka timu maalum kwa ajili ya kuchunguza uharibifu wa reli iliyojengwa na Serikali kwenye kiwanda cha kuzalisha Nondo cha Kilua kilichopo Mlandizi Mkoani Pwani.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Amesema kuwa Serikali iliamua kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli katika kiwanda hicho ili kurahisisha usafirishaji wa nondo kutoka kiwandani hapo kwenda katika maeneo mbalimbali nchini kupitia reli ya kati.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu Novemba 15, 2021) wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha nondo cha Kilua kilichopo Mlandizi Mkoani Pwani.

“Kampuni yenyewe ndiyo iliyoandika barua kuomba reli na Serikali ilitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli kwenye kiwanda hiki, lakini mmeamua kuiua na kuijengea zege na vyuma vingine mmechukua”

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji ili kuhakikisha wanafaidika kutokana na shughuli zao za uwekezaji hapa nchini.

Tazama Video hapo chini