Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza katika ziara yake ya siku saba mkoani Mwanza ambapo amewasisitiza walimu wasijiingize katika masuala ya michango bali wajikite na taaluma.
Waziri Mkuu Majaliwa katika siku yake ya kwanza mkoani humo akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, amezindua madarasa manne ya kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Nyehunge wilayani sengerema huko na kutoa maagizo hayo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa ameshtukia ubadhirifu katika mradi wa Maji ambao unasimamia na halmashauri mbili za wilaya ya Sengerema na Buchosa ambapo ametoa maagizo kwa TAKUKURU kuweza kuchunguza juu ya mradi huo.

