Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman
Akiongea katika ufunguzi wa mafunzo hayo Jaji mkuu Othman Chande amesema kuwa wamefikia hatua hiyo sababu uchaguzi wa mwaka huu unaonekana kuwa na mihemko mingi na wanatarajia kesi nyingi zinaweza kujitokeza pia.
Kwa upande wake mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva amepongeza mtandao wa walinzi wa haki za binaadamu kwa kuandaa mafunzi hayo kwani utakuwa msaada mkubwa kwa walalamikaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka endapo watakuwa na malalamiko yoyote.
Pia Jaji Lubuva ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa sheria inawataka wapiga kura kukaa mita mia mbili baada ya kupiga kura lakini tume kwa kutumia kifungu cha 124A imeelekeza kuwa watu wasikae karibu na vituo ili kuepusha vurugu zisizo za lazima na kama kuna mabadiliko yoyote ya sheria hiyo, mahakama ndiyo itakayo amua.
Msikilize hapa Jaji Damian Lubuva akifafanua mbele ya vyombo vya habari..........