JAJI Edward Rutakangwa akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othmani Chande amesema ili kuepukanana kesi nyingi za kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu ujao nchini Tanzania, ni vyema Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) ikatangaza mapema matokeo mara tu yanapopatikana.
Akifungua mkutano wa majaji leo Jijini Dar es Salaam kwa Niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Edward Rutakangwa amesema kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi kutasababisha mmoja wa waombea kuhisi kama anafanyiwa hujuma mbaya ya kunyimwa haki yake ya kuchaguliwa.
Jaji Rutakangwa amesema kupitia mkutano huo ulioandaliwa na UNDP majaji wa Tanzania sasa wataweweza kujipanga katika kufanya maamuzi ya kisheria pale kesi zinazotokana na kupingwa matokeo ya uchaguzi zitakapojitokeza baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.