
jaji Mstaafu
Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Mkuu wa Tanzania Jaji Mohamed Chande Othman wakati wa kumuaga Jaji wa mahakama ya rufaa aliyestaafu Jaji Engera Kileo baada ya kuhudumu katika mahakama mbalimbali nchini kwa muda wa miaka 40.
Kwa upande wake Jaji Engera Kileo amesema wakati mwingine haki yaweza isitendeke endapo utundu wa kisheria utapewa nafasi kubwa katika uendeshwaji wa kesi, na kuwaasa majaji waliobaki katika tasnia hiyo kujikita katika kutoa elimu kwa wafungwa na wananchi juu ya haki zao ili kuwa na jamii yenye haki na usawa wa kisheria.