Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman.
Jaji Othman amesema hayo jana wakati alipotembelea Maonesho ya 40 ya kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa wameandaa kozi maalumu kwa majaji watakaofanya kazi katika mahakama hiyo itakayoanza Julai 11 hadi 15 mwaka huu.
Jaji Mkuu amesema kuwa kesi ambazo zitaendeshwa katika mahakama hiyo ni zile ambazo upelelezi wake umekamilika ili uamuzi utolewe mapema huku akiongeza kuwa Mahakama hizo zitahusika pia na kesi za ugaidi nchini.
Jaji Othman amesema kuwa baada ya sheria ya Uhujumu uchumi kupitishwa na Bunge imekuwa na marekebisho mengi na kuboreshwa kwa kiasi kikubwa sasa wanasubiri hatua ya rais Dkt. John Magufuli kutia saini ili ianze kutumika.



