Jumamosi , 5th Dec , 2015

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza amewasimamisha kazi watendaji watano wa idara ya ardhi wa halmashauri ya Jiji la Tanga ili kupisha uchunguzi kutokana na utendaji mbovu wa kazi ambao umesababisha jamii kuingia katika migogoro ya ardhi

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza amewasimamisha kazi watendaji watano wa idara ya ardhi na mipango miji wa halmashauri ya Jiji la Tanga ili kupisha uchunguzi kutokana na utendaji mbovu wa kazi ambao umesababisha jamii kuingia katika migogoro ya ardhi na hasara kwa wananchi wa wilaya ya Tanga.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa majumuisho ya ziara aliyoifanya juma hili katika wilaya ya Tanga ambapo amebaini mambo mbalimbali katika maeneo aliyopitia na hatimaye kuona malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya migogoro ya ardhi na kusema kuwa hayuko tayari kuona jamii inayomzunguka haina amani.

Aidha Mahiza amemuagiza Katibu Tawala Msaidizi wa Miundombinu kusimamia suala hilo kuanzia Jumatatu watendaji hao wasiruhusiwe kuingia ofisini na wakakabidhi majukumu yao kwa watumishi wengine ili uchunguzi uanze haraka iwezekanavyo.