Alhamisi , 10th Aug , 2023

Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya leo Agosti 10, 2023 imefikia uamuzi wa kutupilia mbali kesi ya kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya serikali ya Tanzania na ile ya Dubai.

Mawakili pamoja na wananchi waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo

Mahakama imebariki mkataba wa lGA na kusema kuwa ni halali na malalamiko yaliyowasilishwa hayana mashiko.

Kesi hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023 ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya na mawakili wanne ambao ni, Alphonce Lusako, Emmanuel Chengula, Raphael Ngonde na Frank Nyalus.

Akisoma Hukumu hiyo Jaji Dastan Ndunguru amesema baada ya jopo la majaji watatu kusikiliza pande zote mbili mahakama imeamua kuwa hoja zote sita hazina mashiko hivyo kuamua kuwa Mkataba wa IGA hauna dosari za kufanya usitekelezwe.

Akiongea mara baada ya uamuzi wa mahakama hiyo Wakili wa walalamikaji Bonifasi Mwabukusi amesema wanajipanga kwenda kukata rufaa kwani hawajakubaliana na uamuzi wa mahakama.