Jumanne , 27th Mei , 2014

Mahakama ya Kazi Kanda ya Dar es Salaam nchini Tanzania imewamuru kusitisha mgomo na kurejera kazini wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA).

Akitoa amri hiyo Jaji wa Mahakama hiyo Jaji Imani Daudi Aboud amesema Mgomo huo ulioanza Mei 12 haukufuata taratibu na hivyo kuwa ni batili ambapo amewataka wafanyakazi hao kurejea kazini kuanzia hii leo.

Kwa upande wake, Mwenyeketi wa Chama cha wafanyakazi wa TAZARA (TRAWU) Musa Kalala akizungumza na East Africa Radio amesema wamerejea kazini baada ya amri hiyo ya mahakama japo bado hoja ya msingi inayohusu mishahara haijapatiwa ufumbuzi.