Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Christophe Ole Sendeka
Akiongea na East Africa Radio, Ole Sendeka amesema kuwa tatizo la ufisadi nchini lilikuwa limeshamiri kwa kiasi kikubwa hivyo kuundwa kwa Mahakama hiyo kutarudishwa utumishi uliotukuka huku akitaka wananchi kuunga mkono hatua hiyo ya rais Dkt. John Magufuli.
Ole Sendeka amesema kuwa kitendo cha ahadi kutekengewa fungu katika bajeti ya serikali ni hatua moja wapo ya kuelekea kwenye ukamilishaji wa zoezi la kuwa na Mahakama dhidi ya Ufisadi.
Katika hatua nyingine Msemaji huo wa Chama cha Mapinduzi amewataka viongozi wa Vyama vya upinzani wanaotoka bungeni kukaa chini na kutafakari juu ya maamuzi yao kutokana na suala lao wanalolipigania halina mashiko kwa jamii.
Ole Sendeka kitendo cha kulilia Demokrasia kwa kumtuhumu Naibu Spika wakati bado haijathibitika juu ya hoja zao ni kutowatendea haki wananchi wanaowawakilisha na badala yake wangesubiri hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya madai yao.